Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Jeff Sessions amejiuzulu wadhifa wake baada ya kuombwa kufanya hivyo na rais Donald Trump.

Katika barua yake ya kujiuzulu, Sessions amebainisha kuwa uamuzi wa kujiuzulu haukuwa wake na alimjulisha rais Trump kwamba anawasilisha barua kama alivyomuomba.

Aidha, nafasi yake kwasasa itashikiliwa kwa muda na aliyekuwa mkuu wake wa utumishi, Matthew Whitaker, ambapo Whitaker sasa atasimamia uchunguzi wa madai ya Urusi kushirikiana na kampeni za rais Trump mwaka 2016.

Kwa upande wake, mwanachama wa Democratic, Nancy Pelosi anayetarajiwa kuliongoza Baraza la wawakilishi amesema kuwa kujiuzulu huko ni jaribio la wazi la Trump kutaka kumdhoofisha mchunguzi maalumu Robert Mueler anayeongoza uchunguzi ikiwa Urusi ilishirikiana na kampeni za Trump mwaka 2016.

Kiongozi mwingine wa Democratic katika seneti, Chuck Schumer amesema kuwa mabunge yote ya Marekani ni lazima yalinde uchunguzi huo.

 

Video: Sugu ataka viongozi wapimwe akili, Mali kibao za mafisadi zataifishwa
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 8, 2018

Comments

comments