Peter Kibatala ambaye ni mwanasheria wa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ameeleza kusikitikishwa na taarifa zilizosambazwa kuhusu kifo cha mteja wake wikendi iliyopita.

Taarifa za uzushi zilizosambaa hususan kwenye mitandao ya kijamii zilieleza kuwa Askofu Gwajima alifariki dunia wakati akipewa matibau katika hospitali ya TMJ iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Uzushi huo uliutaja ugojwa wa saratani ya damu kuwa chanzo cha kifo cha askofu huyo.

“Nimesikitishwa na taarifa hizi na nimepigiwa simu nyingi sana leo kuniuliza juu ya kifo cha Askofu Gwajima na nimebaki nashangaa kwani ni mzima wa afya,” alisema wakili Kibatala.

Kwa mujibu wa sheria ya makosa ya mtandao, ni kosa kuandika au kusambaza habari zisizo za kweli. Hivyo, mkono wa sheria unaweza kuwashukia walioeneza habairi hizo.

Polisi amtaja aliyemuua 2 Pac Shakur, adai alitumwa na P-Diddy
Rushwa ya Kuku yamtumbua Mtumishi wa Umma