Madaktari wanaomtibu kiongozi wa upinzani nchini Urusi, Alexei Navalny aliyepewa sumu wamesema kuwa amepata fahamu na hali yake tangu alipopatiwa sumu imeimarika.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na madaktari wa Ujerumani, Navalny amekuwa akijibu anachoulizwa na jana Jumatatu hospitali ya Charite, iliyopo mjini Berlin ilisema kwamba Navalny alikuwa anaondolewa polepole mashine inayomsadia kupumua.

Madaktari hao wanasema kwamba mkosoaji huyo wa rais Putin aliwekewa sumu aina ya Novichok kwenye chai alipokuwa hotelini katika uwanja wa ndege wa Tomsk.

Wasaidizi wake wanaishutumu serikali ya rais wa Urusi Vladmir Putin kuhusika na jaribio la mauaji Dhidi ya Navalny madai ambayo serikali ya Putin imekana kuhusika nayo.

Navalny , mwenye umri wa miaka 44 alisafirishwa hadi nchini Ujerumani baada ya kuugua katika ndege moja huko Siberia, mwezi Agosti.

Sven: Kilichotukuta kwa Ihefu FC nilikitarajia
Wasifu (CV) wa Barbara Gonzalez - SIMBA SC