Mwanasiasa mmoja nguli wa nchini Uswisi, Angelo Vukasovic amegeuka kero kwa wengi baada ya kujigamba kwa kupost mtandaoni picha za mizoga na nyama ya wanyamapori akidai kuwa alifurahia kuwinda wanyama hao na kula nyama zao alipokuwa katika ziara ya kitalii nchini Afrika kusini.

Picha hizo zinamuonesha mwanasiasa huyo pamoja na marafiki zake wakiwa na mizoga ya simba, ngiri, pundamilia na wanyama wengine wa porini.

Angelo aliliambia jarida la Aftonbladet kuwa walikula karibu asilimia 80 ya wanyamapori wote waliowawinda na kuwaua. Alidai kuwa walifuata sheria za Afrika Kusini na kupewa idhini na Mamlaka husika kutekeleza uwindaji huo.

“Nilikula asilimia 80 ya wanayama wote niliowaua ikiwa ni pamoja na simba aliyeko kwenye picha. Nyama tamu zaidi ya zote nilizowahi kula ni twiga,” Angelo anakaririwa.

Twiga

Kauli hiyo tata ilikuwa sehemu ya kauli zilizolaaniwa vikali katika siku ya maadhimisho ya Twiga duniani, Juni 21. mmoja kati ya wapinzani wake alisema kuwa kwa kitendo hicho amedhihirisha kuwa anaweza hata kula nyama ya mbwa.

Katika picha nyingine alizopost, aliweka nyama iliyopikwa ambayo alidai ni nyama ya simba.

nyama ya kula

Angelo, mwenye umri wa miaka 41, ni mweka hazina katika chama cha Democrats nchini humo.

Wapishi Wa pizza Watakiwa Kwenda Shule Kusomea Upishi
Magufuli: Tutaufanyia Kazi Mchakato wa Katiba