Aliekuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi uliopita kupitia chama cha CHAUMMA, Mohammed Massoud Rashid, ambae pia ni katibu wa timu ya soka ya Malindi amekuwa mtu wa kwanza kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya makamu wa Urais ZFA Unguja ambapo fomu hiyo amekabidhiwa na mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa ZFA Suleiman Haji “Kibabu”.

Baada ya kuchukua fomu hiyo ya kugombea Makamu wa Urais ZFA Unguja, Massoud amesema amechukua fomu hiyo na akishinda lazima aboreshe soka la Zanzibar.

“Ligi kuu ya Zanzibar ina timu 29, sijapata kuona duniani lakini mimi nikishinda lazima tujenge misingi imara na kuitunza katiba na kuitetea kanuni”. Alisema Massoud.

Wadau wengi wa soka wakiwa na nia ya kuingia katika kinyanganyiro akiwemo kocha wa zamani wa Zanzibar Heroes, Salum Bausi ambae anatarajia siku ya Ijumaa kwenda kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya urais wa ZFA.

Mbali na Bausi pia baadhi ya waandishi wa habari za michezo Jafar Abdallah Ali kutoka ZENJ FM Radio na Masanja Mabula Shauri mwandishi wa kujitegema nao wametangaza nia hiyo, huku wakitarajiwa kugombea nafasi ya Makamu wa rais ZFA Pemba, rais ZFA Unguja na Makamu wa rais ZFA Pemba ambapo mpaka sasa mtu mmoja tu ndie aliekwenda kuchukua fomu ya kugombea katika uchaguzi huo.

Uchaguzi ya chama cha soka Zanzibar (ZFA) unatarajiwa kufanyika tarehe 14 April, huko Kisiwani Pemba ukijumuisha nafasi tatu kugombewa zikiwemo Urais ZFA, Makamu Urais ZFA Pemba.

Martin Demichelis Akumbwa Na Tuhuma Za Kubet
Aliyeteka Ndege ya Misri alichanganyikiwa na ‘Mapenzi’