Mwanasiasa mkongwe nchini Kenya, Kenneth Matiba, ambaye alikuwa mmoja wa wanaharakati wakubwa wa kutetea demokrasia ya vyama vingi nchini humo, amefariki dunia Jumapili usiku akiwa na umri wa miaka 85.

Matiba, ambaye aliwahi kugombea nafasi ya kiti cha urais kupitia chama cha FORD wakati wa utawala wa rais mstaafu Daniel Arap Moi nchini humo na kushika nafasi ya pili, alifariki dunia katika Hospitali ya Karen jijini Nairobi baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Aidha, baada ya kupata habari za kifo chake, rais Uhuru Kenyatta ametuma salamu za rambirambi na kusema kuwa taifa hilo limempoteza mtu mzalendo.

Hata hivyo, Matiba aliwahi kuwekwa kizuizini wakati wa utawala wa Rais mstaafu wa nchi hiyo, Daniel Arap Moi kitu ambacho kilimfanya apooze upande mmoja wa mwili.

 

 

 

 

 

 

Tanzia: Watu 7 wafariki dunia kufuatia mvua zinazonyesha Dar es salaam
JPM afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali