Polisi katika eneo la Bomet nchini Kenya linamshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za kuwaua watoto wake watatu kufuatia ugomvi kati yake na mkewe.

Kwa mujibu wa wanakijiji wa eneo hilo, mwanaume huyo anadaiwa kuwaua wanaye wenye umri wa miaka kumi na mbili, nane na mitano.

Imeelezwa kuwa wanandoa hao walikuwa wakigombana mara kwa mara na ugomvi wao pia ulihusishwa na uhalali wa watoto wao. Mkewe alifanikiwa kukimbia.

Kwa mujibu wa Citizen, Polisi wamesema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Sigor na watafikishwa mahakamani punde baada ya upelelezi kuhusu tukio hilo kukamilika.

Mkuu wa polisi, Mutai Lelaitich ameeleza kuwa upelelezi unaendelea vizuri na kwamba mke wa mtuhumiwa pia ameshapatikana.

Taifa Stars kuweka historia
Video: Waziri afuma simu, mihadarati gerezani, Waislamu kuomba dua ya mvua