Mwanaume mmoja maskini nchini India alibeba maiti ya mkewe kwa zaidi ya kilomita 12 baada ya hospitali alikofariki kushindwa kumsafirisha kwa gari la kubebea wagonjwa hadi kijiji mwake.

Mke wa Dana Mjhi, Amang, mwenye umri wa 42, alifariki dunia baada ya kuugua maradhi ya kifua kikuu katika hospitali ya Ulaya, mji wa Bhawanipatna jimbo la Orissa.

Bwana Mahji alisema kijiji chake kilikuwa umbali wa kilimita 60 na hakuwa na uwezo wa kulipa gharama ya usafiri wa gari la kubebea wagonjwa.Mwanamke huyo alilazwa hospitalini hapo na siku ya Jumanne akawa ameaga dunia.

Mume wa marehemu aliamua kuuchukua mwili wa marehemu mke wake  bila kuwafahamisha wahudumu wa hospitali hiyo,’ Mganga mkuu wa hospital hiyo ”B Brahma alisema

Kwa upande wake Bwana Majhi, anadai mkewe alifariki siku ya Jumanne usiku na kuamua kubeba mwili wake siku ya Jumatano baada ya wahudumu wa hospitali hiyo kumuomba kuondoa mwili huo.

” Nilikuwa nikiwaomba wahudumu wa hospitali hiyo wanisaidie gari nimbebe mke wangu lakini nikaambulia patupu,Kwa sababu mimi ni maskini na nisingeweza kukodisha gari la kibinafsi sikuwa na njia nyingine ila kumbeba mke wangu mabegani”Alisema.

Mapema Jumatano  alifunga mwili wa mkewe na nguo na kuanza safari hiyo ndefu ya kuelekea kijijini kwao Melghar kwaajiri ya kukamilisha mila na tamaduni za mwisho akiungana na mwanawe mwenye umri wa miaka 12 , Chaula.

Alitembea kwa takriban kilomita 12, ndipo watu walipoingilia kati na kumsaidia kwa gari la kubebea wagonjwa  hadi mwisho wa safari yake na Shughuli za kimila za kuchoma mwili wa marehemu mkewe ilifanyika siku ya Jumatano usiku

Video: Ukawa, ACT-Wazalendo washauri Rais Magufuli afute vyama vyote vya siasa
Mapigano Kusitishwa Rasmi Jumatatu Nchini Colombia