Kufuatia tafiti zilizofanywa na wanasayansi wamebainisha kuwa endapo mwanaume atapata rafiki/mpenzi mwenye sifa na tabia hizi inashauriwa asiruhusu aende au kuachana nae, kuchagua rafiki wa kike wa kuishi nae maisha yako yote si kazi rahisi kama ambavyo inadhaniwa.

Japokuwa muda mwingine watu hufikiri zaidi juu ya muonekano wa mtu, hata hivyo ni muhimu kufahamu kuna sifa nyingine muhimu zaidi ya huo muonekano na unatakiwa kuzizingatia itakufanya maisha yako kuwa bora.

Ukikutana na mwanamke mwenye sifa/ tabia hizi usimwache aende, mng’ang’anie mpaka mwisho.

  1. Mwenye akili zaidi yako

Hii inafanya akili ya mwanaume ifanye kazi kwa haraka na wakati wote na kufanya akili ya mwanaume kukua na kutanuka, matatizo mengi ya ubongo yanaweza kutatuliwa endapo utaishi na mwenza mwenye utashi zaidi yako kwani atakuwa mwenye kukupa changamoto mbalimbali zitazokufikirisha namna ya kuzitatua na kukabiliana nazo bila kukata tamaa.

2. Mwaminfu/Mkweli/Muwazi

Hii ni tabia ambayo wanawake wachache sana wamebahatika kuwa nayo, wengi sio wa kweli/wawazi/waaminifu  kwa mlengo wa kujilinda wenyewe mara zote wanataka kuonekana ni watu wazuri hivyo muda mwingine hupendelea kudanganya ili waonekane wema na hawakosei endapo utakutana na mwanamke mwenye tabia hii ya dhahabu usimwache aende kwani utakuwa umepoteza kitu kikubwa sana maishani mwako kama inavyofahamika madhara ya kuwa na mtu asiyeaminika.

3. Mtazamo chanya

Mwanamke mwenye mtazamo chanya anaweza kukutia nguvu au kukushauri kuwa mtu bora na chanya zaidi, unaweza kumjua mwanamke mwenye mtazamo chanya kupitia mawazo anayokupa juu ya mambo mbalimbali.

   4. Kufurahia utani wako

Mwanaume yeyote hupenda mwanamke ambaye hufurahi pindi amtaniapo, watafiti wanasema kuwa mwanamke mzuri ni yule anayeelewa kile anachozungumza mwanaume wake, japokuwa kuna matani mengine hayafurahishi ni umakini tu kama unafanya kwa lengo la kumfurahisha mwenza basi fanya kweli usitegemee kufanya utani utakao mkasirisha akafurahi.

5. Muwazi

Mwanamke anayeweza kuwa muwazi kwa kuongea mawazo na hisia zake kwa mwanaume ni mwanamke anayemvutai sana mwanaume, hii inamfanya mwanaume ajisikie anaumuhimu katika maisha yake na hii ina maanisha kuwa mwanamke ana imani na mwanaume huyo, mara chache sana wanawake hutoa taarifa zao binafsi mpaka awe amependa, lakini pia mwanaume naye lazima aonyeshe ushirikiano wake kwani ukiwa mtu wa kukatisha tamaa na kuona mambo hayawezekani inafanya siku nyingine mtu asikuamini na kukushirikisha katika mawazo yake.

6. Msaidizi

Mwanamke utakayemchagua lazima awe ni yule anayekushika mkono katika nyakati zote, hapa mwanaume lazima atambue na kukiri mchango anaopewa na mwanamke wake hii inasaidia sana kuimarisha penzi.

7. Mwenye mahusiano mazuri na wazazi

Hii ni muhimu sana kwani inaonyesha jinsi gani mwamke huyi anaheshima na kutambua majukumu yake katika malezi.

8. Mwenye upole na ukarimu.

 

 

 

 

 

IGP Sirro afanya mabadiliko ndani ya Jeshi la Polisi
Simon Mignolet kuondoka Anfield

Comments

comments