Mwandishi wa habari wa Al Jazeera Shireen Abu Akleh (51) ameuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa akiwa katika majukumu yake ya kazi ya kufuatilia uvamizi wa Jeshi la Israel kwenye kambi ya wakimbizi ya Jenin, Palestina.

Kwa mujibu wa Al Jazeera, mpaka sasa inavishutumu vikosi vya usalama vya Israel kwa kumlenga na kumuua kwa makusudi Abu Akleh na kuitaka jumuiya ya kimataifa kulaani na kuiwajibisha Israel.

Wakati anapopigwa Risasi hiyo Akhel alikua amevalia kitambulisho cha waandishi wa habari na alikimbizwa hospitali ya jiji ya Jenin ambapo madaktari ndio walitoa taarifa ya kifo chake.

Mwandishi mwingine wa habari wa Palestina, Ali al-Samoudi pia alijeruhiwa mgongoni lakini hali yake inaendelea vizuri.

Jeshi la Ulinzi la Israel limedai kuwa vikosi vyake vya usalama vimekuwa vikifanya kazi katika eneo hilo kuwakamata washukiwa wa matukio ya kigaidi,” na washukiwa wa Kipalestina na wanajeshi wa Israel wote walikuwa wakifyatua risasi wakati huo.

PANYA ROAD watikisa Baraza la Madiwani Biharamulo
Joash Onyango mambo safi Simba SC