Mwandishi wa Habari wa ITV na Radio One mkoani Songwe Gabriel Kandonga, amefariki dunia kwa ajali ya gari.

Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Septemba 24, 2021, wakati akitokea nyumbani kwake Mpemba kuelekea wilayani Songwe katika majukumu yake ya kila siku.

Mkuu wa mkoa wa Songwe Omary Mgumba, amethibitisha kutokea kwa kifo cha mwandishi huyo na kusema ajali hiyo imetokea katika eneo la shule ya Sekondari Mlowo ambapo alikuwa anajaribu kulipita lori na hatimaye kulivaa fuso kwa upande wa nyuma.

Jamhuri yafunga ushahidi wake kesi ndogo ya Mbowe na wenzake
Watatu wakamatwa kwa utekaji nyara