Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amepiga marufuku kwa abiria yoyote anayeingia na kutoka mkoani humo kuingia kwenye usafiri wa umma bila kuvaa barakoa.

Mwanri ametoa maagizo hayo kwenye kikao kazi kilichokutanisha wakuu wa wilaya, wakurugenzi na waganga wakuu kutathmini mwenendo na udhibiti wa maambukizi ya Virusi vya Corona 

“Mtu anasema Corona oyee tutakuzibua sisi tunakuja na kitu kinaitwa kubamiza Corona” Amesema Mwanri .

Hata hivyo amewataka wakuu wa wilaya kuhakikisha vitendea kazi vinavyotumika kupambana na Corona kuuzwa bei ambayo mwananchi wa kawaida anaweza kuimudu.

Mkuu huyo wa mkoa amewataka wananchi kuchukua tahadhari juu ya janga hili kwa kufuata maelekezo yanayotolea na wizara ya afya.

Man Utd yawaita walio nje ya England
Uturuki: Tupo tayari kwa fainali Ligi Ya Mabingwa