Mjasiriamali na Mwanzilishi wa programu ya antivirus ya McAfee, John McAfee amefariki dunia akiwa gerezani katika Jiji la Barcelona nchini Uhispania.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, McAfee alikutwa akiwa amefariki ndani ya chumba alichokuwa akiishi gerezani hapo.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa kuna uwezekano kuwa McAfee alijiua ingawa Afisa wa mmoja wa serikali aliiambia Associsted press kuwa bado sababu ya kifo inachunguzwa.

Umauti umemkuta saa chache baada ya Mahakama nchini humo kuamua kumsafirisha hadi Marekani ili akashtakiwe kwa makosa ya kukwepa kodi.

McAfee alikamatwa kwenye uwanja wa ndege huko Barcelona Oktoba, 2020 na  iwapo angekutwa na hatia katika mashtaka hayo ya jinai yanayohusiana na ushuru, angekabiliwa na kifungo cha hadi miaka 30.

Magari sita ya abiria yakamatwa na msiba feki Morogoro
Amuua mama mkwe alipojaribu kumsuluhisha na mkewe