Mabingwa wa soka nchini Ufaransa, Paris Saint-Germain wameendelea kuwa katika mipango ya kuweka rekodi ya usajili duniani huku macho yao yakiwa yamegeuzwa kwa mchezaji bora wa dunia kwa sasa Cristiano Ronaldo.

PSG wametajwa kuwa katika mipango ya kutaka kusamjili mshambuliaji huyo kwa ada ya usajili wa paund million 87.3 kutokana na hitaji la tajiri wao Nasser Al-Khelaifi la kutaka kumuona Ronaldo akitua Parc des Princes.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti la The Sunday Times umebaini kuwepo kwa mipango hiyo ambayo inapewa msukumo ili ikamilishwe mwishoni mwa msimu huu.

Ada hiyo ya usajili ni sehemu ya pesa iliyotengwa inayokadiriwa kufikia paund million 250 ambazo pia zinajumuisha mshahara wake atakaolipwa kwa juma endapo atakamilisha mpango wa kuelekea jijini Paris.

Hata hivyo uchunguzi huo umebaini kwamba, huenda PSG wakapata wakati mgumu wa kumng’oa Ronaldo nchini Hispania, kutokana na kiasi cha pesa walichokitenga kwa shughuli ya uhamisho wake, na huenda viongozi wa Real Madrid  wakahitaji pasa zaidi.

Ronaldo ama wakala wake bado hawajazungumza lolote kuhusu jambo hilo mpaka sasa, japo wapambe wao wamekua wakitoa ushirikiano katika vyombo vya habari.

Ronaldo alisajiliwa na Real Madrid, mwaka 2009 akitokea Man Utd kwa ada ya uhamisho wa paund million 80, iliyoweka rekodi duniani kwa miaka minne na baada ya hapo usajili wa mashambuliaji wa pembeni kutoka nchini Wales Gareth Bale wa paund million 85.3 uliweka rekodi mpya akitokea Tottenham Hotspurs.

Tenga: Sitowania Tena Urais CECAFA
Sumaye Aeleza Atakuwa ‘Nani’ Baada Ya Uchaguzi Mkuu