Halmashauri ya jiji la Dar es salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha Mabasi yaendayo haraka Udart kilichopo jangwani na kuhamishia  kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo (UBT).

Hatua hiyo ni kutokana na eneo hilo la jangwani kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika kwa magari hayo.

Kufuatia kikao cha kawaida kilichofanyika jana cha  Madiwani, Meya wa jiji la Dar es salaam, Isaya  Mwita amesema uamuzi huo umefikiwa kunusuru magari hayo yasiendelee kuharika.

Menejimenti ya kampuni ya UDART na viongozi wa jiji wapo kwenye majadiliano kuhusu suala hilo waweze kufikia mwafaka.

”kwa sasa tupo kwenye majadiliano kwa ajili ya  kuhamisha kituo cha mabasi yaendeyo kasi UDART cha Jangwani tuweze kukipeleka Ubungo kwa sababu eneo la jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara mvua 0inapomyesha alisema Mwita.

Alisema suala hilo linaendelea  kufanyiwa kazi na Haslmashauri ya jiji hilo ipo kwenye mchakato wa kupanua Mto Msimbazi uweze kuwa na nafasi kubwa ya kusafirisha maji hadi baharini.

Aidha kufuatia mvua zilizokuwa zinaendelea kunyesha jijini Dar es salaam, Jangwani ni moja ya eneo ambalo mara kwa mara limekuwa likikumbwa na mafuriko na kupelekea safari za mabasi ya mwendokasi kuhairishwa, aidha kufuatia mvua zilizonyesha siku tatu zilizopita zimepelekea mabasi 29 kati 140 kuharibika na na kufanya baadhi ya wafanyakazi kupewa likizo mpaka marekebisho yatakapokamilika.

TMA yatabiri ujio wa mvua kubwa kwa siku tano
Lusinde adai serikali imeshindwa kudhibiti matumizi ya fedha