Mwenge wa uhuru umepokelewa Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam na Mkuu wa Wilaya hiyo, Sophia Mjema ambapo unatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali katika wilaya hiyo.

Akizungumza katika mapokezi hayo, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Msongela Palela amesema kuwa miradi itakayozinduliwa ni pamoja na ule endelevu wa uboreshaji mandhali ya mji ambapo mradi huo utakuwa ni kumbukumbu katika uboreshaji wa mandhali.

Amesema kuwa katika kutekeleza miradi ya uboreshaji mji na upandaji miti Manispaa hiyo imekumbana na changamoto  ya wananchi kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu utunzaji wa mazingira.

Hata hivyo, Mkurugenzi huyo amemuomba kiongozi wa mbio za mwenge kuweka jiwe la msingi ikiwa ni sehemu ya uboreshaji ya mandhari ya mji ikiwa ni zoezi endelevu kwa maeneo mengine ya Manispaa ya Ilala.

Magazeti ya Tanzania leo Mei 30, 2017
Picha 15: Mbio za Mwenge wa Uhuru Ilala, Dar es salaam

Comments

comments