Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini, Ephraim Mwaitenda amenusurika kifo baada ya kupigwa risasi mgongoni na watu wasiojulikana.
Mwaitenda ambaye kwa sasa amelazwa kwenye hospitali ya Rufaa Mbeya akiendelea na matibabu,alipigwa risasi akiwa amelala usiku wa manane kibandani shambani kwake Kyela.
Aidha,Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo,amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29. 01. 2017 majira ya saa 05. 45 usiku katika kitongoji cha Ilopa, Kijiji cha Mahenge, Kata ya Makwele, Tarafa ya Ntebela, wilayani Kyela Mkoa wa Mbeya.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha bunduki iliyotumika katika shambulio hilo ni ya kienyeji kwani risasi zilizotumika ni za golori na kama ingekuwa bunduki za kisasa asinge nusurika,”amesema Kamanda Lukula.
Hata hivyo Kaimu Kamanda Lukula amesema kuwa hakuna mtu anayeshikiliwa ingawa hatua za awali zinaonyesha huenda shambulio hilo lilifanywa na watu wa karibu na Mwenyekiti huyo.

Video: Ugomvi wa DC, mbunge watua kwa Waziri Mkuu, Vijana wa CCM wamuonya Seif
Makamu Wa Rais Ghana Awapongeza Black Stars