Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James, amepata ajali  kwenye msafara wake Wilayani Meatu Mkoani Simiyu alipokuwa akitoka Mkoani humo kuelekea Shinyanga.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu, ACP Boniventure Mshongi, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akieleza kuwa ni ajali ndogo ya kawaida ambayo imesababishwa na vumbi kuzidi hali iliyopelekea gari moja kwenye msafara huo kugonga basi la abiria kwa nyuma.

”Ni kweli ajali hiyo imeripotiwa kwangu ila kwasasa nipo kwenye majukumu mengine na mkuu wa majeshi lakini taarifa nilizo nazo ajali imetokea na ni ya kawaida, hakuna mtu aliyepoteza maisha au kujeruhiwa vibaya, nitakapopata taarifa kamili nitawaeleza,”amesema Kamanda.

Hata hivyo, Kamanda Mshongi, ameongeza kuwa msafara huo ambao ulikuwa kwenye mwendokasi, ulizidiwa na vumbi kutokana na barabara za vumbi hivyo kusababisha gari hilo kugonga basi kwa nyuma lakini haikuleta madhara makubwa.

Wanachama Yanga wapinga kujiuzulu kwa Manji
Simba: Ni lazima tukawachape Everton, Gor Mahia hawana kitu