Seneta wa Garissa nchini Kenya Mohamed Yusuf Haji amefariki dunia katika hospitali ya Aga Khan, mjini Nairobi ambako alikuwa anapata matibabu, kwa mujibu wa familia yake.

Yusuf Haji amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.

Haji pia alikuwa mwenyekiti wa Jopo la kazi la Maridhiano nchini Kenya maarufu kama BBI (Building Bridges Initiative).

Haji alijiunga na utawala wa maeneo nchini Kenya mwaka 1960 kama Mkuu wa Wilaya na kupanda ngazi hadi kuwa miongoni mwa makamishna maarufu mikoani.

Haji alistaafu katika uongozi wa Utawala wa mikoa mwaka 1998.

Mwaka 2002, aliteuliwa kuwa mbunge na mwaka 2007, akachaguliwa kama Mbunge wa eneo la Ijara kwa tiketi ya chama cha Kenya African National Union (KANU).

Mpaka umauti unamkuta Haji alikuwa anahudumu muhula wake wa pili kama Seneta wa Garissa.

Hofu yatanda kuibuka kwa janga la ebola
Kim Paulsen kocha mpya Taifa Stars