Aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo ameuawa kikatili na watu wasiojulikana.

Taarifa kutoka mkoani humo zimeeleza kuwa kiongozi huyo wa Chadema aliuawa kwa kupigwa na vitu vizito na vitu vyenye ncha kali na watu wasiojulikana.

Alphonce Mawazo, Mwenyekiti Chadema

Mwenyekiti huyo wa Chadema alikuwa mgombea ubunge wa jimbo la Busanda na inadaiwa kuwa jana alikuwa katika kikao cha maandalizi ya kuendelea kumnadi mgombea udiwani wa chama hicho saa chache kabla ya kuvamiwa na kundi la watu

Taarifa zinaeleza kuwa wakati kikao cha Chadema kinaendelea lilikuja kundi la vijana kama kumi ambao walikaa nje ya ukumbi huo na baadaye walianzisha fujo. Watu waliokuwa kwenye chumba hicho cha mkutano walitoka na kuanza kupambana na vijana hao lakini hali ilivyoendelea kuwa ngumu, marehemu anadaiwa kuwa alikimbia kutoka kwenye eneo hilo.

Hata hivyo, alifuatwa na watu wenye gari ambalo namba yake bado haijafahamika ambao wanadaiwa kumkamata na kumpiga na kitu chenye ncha kali kichwani na kumuacha akiwa na hali mbaya. Mawazo alikimbizwa hospitali lakini alipoteza maisha muda mfupi baadaye.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alituma salamu za rambirambi kwa wanachama wa chama hicho kufuatia kuuawa kwa Mawazo na kuvitaka vyombo vya usalama kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.

“Tunavitaka vyombo vya dola vitupe taarifa kamili ya wahusika wa unyama huu. Nawapa pole wanachadema wote, ndugu jamaa na marafiki,” alisema Mbowe.

 

 

 

 

 

Madeko ya Kanye West Yampa Mawazo Kim Kardashian Kuhusu Mtoto wa Pili
Mwanamke Aliyemuua Mwanae Kwa 'Kumuoka' Kwenye Oven Ahukumiwa