Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa CCM wilaya ya Arusha, Vicky Mollel ametangaza kukihama chama hicho na kuhamia Chadema.

Akizungumzia uamuzi wake, Vicky ameeleza kuwa amechukua uamuzi huo baada ya kuchoka na majungu yaliyo ndani ya chama hicho ambayo amedai kuwa yanasababisha kuishi kwa kuogopa watu fulani badala ya kufuata katiba.

“Nilipokaa niliona nadhoofisha kipaji changu kwa kumuogopa mwanadamu kwani ninachoamini ni kuwa chama kinaongozwa na katiba na kanuni. Lakini badala yake watu wachache wanaongoza CCM huku wakidhani siasa ni kuzusha majungu na chuki,” Mollel aliwaambia waandishi wa habari.

Aliongeza kuwa chama hicho hivi sasa kinatumia muda mwingi kutafuta mchawi na nani aliyekihujumu na kwamba mwenendo huo ulimkatisha tamaa.

Mollel anatarajiwa kukabidhiwa kadi ya Chadema Jumatano wiki hii na aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa.

Mollel ambaye aliwahi kuwa diwani wa viti maalum, alimtaka Godbless Lema (Mgombea ubunge kupitia Chadema) kusahau tofauti zilizokuwepo kati yao huku akieleza kuwa hakuna urafiki wala uadui wa kudumu katika siasa.

Pia, aliwashukuru akina mama na wafuasi wa CCM waliokuwa wanamuunga mkono huku akiwaomba wamfuate Chadema.

Mawaziri Wa JK Watajwa majina ya Mawaziri wa Magufuli yaliyovuja
TRA Yaishukia Bakwata, Yaipa Siku Saba Kuwasilisha Nyaraka