Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa Selestine leo amefungua kozi ya walimu wa mpira wa miguu ngazi ya chini (Grassroots) inayofayika katika ukumbi wa TFF uliopo Karume jijini Dar es slaam.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa kozi hiyo ya siku tano, Mwesigwa amewaomba washiriki kuitumia vizuri nafasi hiyo waliyoipata kwa kwenda kuwafundisha na kuupenda mpira wa miguu watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 6-12.

Mwesigwa amewaomba walimu hao kutoka shule za msingi za mikoa ya Dar es salaam, Mtwara, Lindi na Ruvuma kusaidia katika kukuza mpira wa miguu ambao chimbuko lake ni watoto wadogo kuupenda na kuucheza mpira huo.

Jumla ya washiriki 30 kutoka mikoa minne wanashiriki kozi hiyo, inayoendeshwa na mkufunzi wa FIFA kutoka nchini Mauritius, Govinden Thondoo ambaye ametoa pongezi kwa TFF kwa kuwa na maendeleo mazuri katika kozi ya Grassoot kulinganisha na nchi nyingine zilizopo katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati wneye jumla ya nchi 15.

Jumla ya walimu 106 kutoka katika shule za msingi za mikoa mbalimbali nchini Tanzania zina makocha waliopata kozi za Grassoort katika kipindi cha miaka 2, na lengo likiwa ni kufikisha walimu 25,000.

 

FA Cup Kuendelea Leo
Joh Makini: Tusiamini Katika Kuwashirikisha Wasanii Wa Kimataifa Kuwa Wa Kimataifa