Shirikisho la soka nchini TFF limesema hivi sasa wanaangalia zaidi maendeleo ya timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania Serengeti Boys na siyo kuvutana juu ya umri wa mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ya Congo Brazzaville.

Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Celestine amesema, suala la mchezaji huyo wameliacha chini ya Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF ambapo wameagiza mchezaji huyo kufanyiwa upya vipimo ambavyo hapo awali Namibia walishindwa kutokana na gharama ambazo walitakiwa kuzilipia wao wenyewe.

Mwesigwa amesema, mchezaji huyo anadaiwa kuwa na umri zaidi ya ule unaotakiwa na alivaa namba 05 katika mchezo wa timu ya Taifa ya Namibia dhidi ya Timu yake ya Congo Brazzaville na katika mchezo dhidi ya Serengeti Boys alivaa jezi namba 10 huku katika mchezo wa mwisho ambao Congo walifanikiwa kufuzu kuelekea katika fainali za Mataifa ya Afrika kwa kuichapa Serengeti Boys bao 1-0.

 

Video: Sababu za kuongezeka kwa magonjwa
Majaliwa apokea sh. mil. 5 kwa ajili ya waathirika wa tetemeko Kagera