Mwigizaji Tommy Lister wa nchini Marekani maarufu ‘Tiny’ amefariki dunia, ambapo kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa  imeripotiwa kwamba alikutwa akiwa na hali mbaya kwenye nyumba  aliyokua anaishi na kuwahishwa hospitali alikofia.

Polisi wa Los Angeles wamesema marafiki zake walipatwa na wasiwasi kwa ukimya wake tangu walipoachana naye siku ya Jumatano na baadaye walivyofatilia wakakuta amefariki.

Pamoja na kwamba utafanyika uchunguzi, Polisi wamesema wanaamini kifo chake ni cha kawaida na hawadhani kama aliuwawa.

Lister ambaye amecheza kwenye filamu mbalimbali ikiwemo ya FRIDAY akitumia jina la Deebo, amefariki akiwa na umri wa miaka 62.

Kocha Mwadui FC aitangazia vita Young Africans
Dimpoz alamba dili South Africa