Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba amewaonya wanaopanga kuandamana kuwa watashughulikiwa kwa kupanga mauaji.

Akizungumza leo katika uzinduzi wa kiwanda cha mafuta ya alizeti mkoani Singida ambapo Rais John Magufuli ndiye mgeni rasmi, Dkt. Nchemba amesema kuwa wanaopanga maandamano wana lengo la kutaka Serikali ifyatue risasi ili wachafue taswira ya nchi.

Hivyo, ameonya kuwa mtu yeyote atakayeandamana hata nyumbani kwake kuzunguka kitanda na akasababisha mtu yeyote kuumia atashughulikiwa.

“Hakuna maandamano, hakutakuwa na atakayeandamana. Na ikatokea hata watu wakaandamana ndani ya nyumba kuzunguka kitanda mmoja akaumia, huyo aliyewaita waandamane atashughulikiwa,” amesema Dkt. Mwigulu Nchemba.

Alimhakikishia Rais Magufuli kuwa hakuna atakayeandamana na kwamba ametoa maelekezo kwa jeshi la polisi kuwachukulia hatua wanaopanga kuandamana kwani lengo lao ni ovu dhidi ya taswira ya taifa.

JPM: Sitishwi wala sitishiki, niko kwa ajili ya Watanzania
Mbunge wa CCM ajitosa jimbo la Lissu, aanza kutoa misaada