Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha  Septemba 10, 2020 imepitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa za wagombea ubunge na Udiwani zilizowasilishwa na wagombea kupitia kwa wasimamizi mbalimbali wa Uchaguzi nchi nzima.

Rufaa hizo zimewasilishwa chini ya kifungu cha 40(6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 kikisomwa pamoja na kifungu cha 44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ambacho kinatoa fursa kwa wagombea wa Ubunge na Udiwani kukata rufaa wanapokuwa hawajaridhika na uamuzi wa wasimamizi wa uchaguzi kutokana na pingamizi zilizowasilishwa.

Katika kikao hicho, Tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi jumla ya rufaa 60 kati ya hizo rufaa 2 ni za wagombea ubunge na 58 ni za wagombea udiwani.

Tume imekubali rufaa moja na kumrejesha mgombea katika orodha ya wagombea kutoka jimbo la Iramba Magharibi huku ikikataa rufaa moja ya mgombea ambaye uteuzi wake ulitenguliwa kutoka jimbo la Iramba Magharibi.

Aidha, Tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 58 za Madiwani, ambapo imekubali rufaa 34 na kuwarejesha wagombea katika orodha ya wagombea Udiwani.

Rufaa hizo ni kutoka kwenye Kata za Kahororo(Bukoba), Ishozi(Nkenge), Chongoleani (Tanga Jiji),  Kirare (Tanga Jiji), Mwamanga (Magu), NgÊ»haya (Magu), Riroda (Babati Vijini), Maswa Magharibi (Maswa), Kirumba (Ilemela), Bonga (Babati Vijini), Kamagambo (Karagwe), Namelock (Kiteto), Masewa (Bariadi), Bweranyange (Karagwe), Kituntu (Karagwe), Kamagambo (Karagwe), Msowero (Kilosa), Lubugu (Magu), Lingeta (Meatu), Ifakara (Kilombero), Kiloli (Sikonge), Mkoma (Rorya), Nyamhongolo (Ilemela), Sikonge (Sikonge), Tanganyika (Muheza), Uhenga (Wanging’ombe), Babati (Babati), Vwawa (Mbozi), Lukanga (Mkuranga), Langai (Simanjiro), Lutale (Magu), Majohe (Ilala), Namabengo (Namtumbo) na Viwanja Sitini (Kilombero).

Tume imekataa rufaa 23 za wagombea ambao hawakuteuliwa. Rufaa hizo ni kutoka kwenye Kata za Ilemela (Ilemela), Kayenze (Mwanza Jiji), Kiarare (Tanga Jiji), Mabawa (Tanga Jiji), Ilemela (Ilemela), Kadoto (Maswa Magharibi), Iyela (Mbeya Jiji), Kirua Vunjo Magharibi (Vunjo), Mji Mpya (Morogoro Mjini), Pugu (Ukonga), Tembela (Mbeya Mji), Vikumburu (Kisarawe), Mecco (Ilemela), Kibara (Mwibara), Kiloleli (Sikonge), Changarawe (Mafinga Mji), Igawilo (Mbeya Mjini), Msonga (Mkuranga), Uru Kaskazini (Moshi Vijini), Kivukoni (Ilala), Maanga (Mbeya Mjini), Nsalaga (Mbeya Mjini) na Jangwani (Ilala).

NEC imekataa rufaa moja ya kupinga walioteuliwa kutoka kata ya Arri (Babati Vijijini).

Idadi hii inafanya jumla ya rufaa za wagombea Ubunge zilizofanyiwa uamuzi na Tume kufikia 113 na za wagombea Udiwani 103. Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku. Wahusika wa rufaa hizo watajulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa Tume.

50 wahofiwa kufariki kwa kuangukiwa na mgodi wa dhahabu DRC
Rais Maduro: Tumemkamata komando wa Marekani