Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo zimeshikiliwa kwa mda mrefu na zina makosa madogo na kutaka wasikae nazo kwa mda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu.

Mwigulu amesema pikipiki zenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita, madawa ya kulevya na wale wanaotelekeza wabaki nazo na wafanye utaratibu wa kuwapeleka mahakamani au kuzitelekeza.

Amesema kwamba pikipiki zenye makosa madogo wafanye mpango wa kuyatatua haraka na kuwarudishia ikiwezekana pia wahusike na kuwapa elimu juu ya makosa yao ili wayafanyie marekebisho.

”Wapeni masomo wamekosea wapi waelekezeni na waliowabishi warekebisheni lakini tusirundike tukatengeneza vyuma chakavu kwa hivi vitu ambavyo utatuzi wake tunao, tutumie huu mkono kutatua kwa yale ambayo yapo ndani ya mamlaka yetu” amesema Mwigulu.

Amesema kuwa ipo haja ya vijana sasa kufundishwa zaidi kuhusu sheria ya usalama barabarani ili kupunguza ajali ya pikipiki na mrundikano wa pikipiki katika vituo vya polisi nchini kwani kila anapopita vituo vya polisi hukuta pikipiki ni nyingi na makosa yao ni madogo.

Zingatia yafuatayo kupata pasi ya kusafiria ya kielektroniki
Masauni atoa ufafanuzi kuhusu askari wanojichukulia sheria mkononi