Katika kutekeleza ahadi ya Rais Magufuli kuwa mawaziri wake watakuwa kazini muda wote, Waziri wa Kilimo na Mifugo, Mwigulu Nchemba jana alishtukiza katika machinjio ya Ukonga Mazizi jijini Dar es Salaam, majir aya saa saba usiku.

Ziara hiyo ya kushtukiza ambayo haikutegemewa kabisa ilizaa matunda baada ya Waziri Nchemba kubaini ng’ombe walioingizwa kimagendo na kukwepa kulipa ushuru.

Nchemba 2

Waziri huo alikamata jumla ya ng’ombe 180 waliokuwa wanaingizwa katika machinjio hayo bila kibali cha serikali na bila kulipiwa ushuru. Hao walikuwa miongoni mwa ng’ombe 200 waliokuwa waliongizwa usiku huo. Hivyo, ni ng’ombe 20 pekee waliokuwa na kibali.

Kufuatia maovu hayo yaliyobainika, Waziri Nchemba aliwatimua katika nafasi za uongozi wote waliokuwa na nafasiza uongozi katika machinjio hayo, na kuagiza vyomba vya usalama kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika.

 

Waliodungua Helkopita Wapigwa jumla ya miaka 60 jela haraka
Maalim Seif ailima ZEC barua