Msanii wa maigizo, Barton Mwemba maarufu kama Mwijaku amemtupia dongo  Emmanuel Mathias ambaye ni mchekeshaji na mshereheshaji maarufu kwa jina la Mc Pilipili akidai kuwa yeye ni zuzu.

Dongo hilo ni kufuatia kitendo cha Mc Pilipili kulia wakati wa sherehe ya kumvalisha pete mchumba wake Filomena, tukio ambalo lilikuwa gumzo kwa siku kadhaa.

Mwijaku amedai kuwa Mc Pilipili ni zuzu kwenye mapenzi na kwamba amewadhalilisha wanaume wa jiji la Dar es Salaam kwa kufanya kitendo hicho

Hata hivyo, Msanii huyo ambaye ni rafiki wa sanaa wa Mchekeshaji huyo alisema, “sio dhambi kulia ila ni dhambi kubwa mwanaume kulia mbele za watu kwa ajili ya mwanamke’’.

Msanii huyo ameeleza kile alichodai kuwa anamfahamu vizuri MC Pilipili na amewahi kumueleza mengi kuhusu uhusiano wake wa mapenzi.

Angalia video hii kupata undani wa alichokuwa akizungumza pamoja kama marafiki kuhusu masuala ya mahusiano ya mapenzi na wanawake aliowahi kuwa na uhusiano nao.

Wakulima mkoani Njombe watakiwa kuachana na kilimo cha mazoea
Mwanamitindo maarufu auawa siku chache kabla ya harusi yake

Comments

comments