Binti mmoja, Ashika Nur Fauziah (7), ambaye waokoaji walifanya juhudi za siku nzima kujaribu kumnusuru baada ya tetemeko la ardhi lililowauwa mamia ya watu huko Java Magharibi nchini Indonesia, amepatikana akiwa amefariki.

Waokoaji hao, wanasema waliupata mwili wa Ashika chini ya vifusi katika eneo la Wilaya iliyoathirika zaidi kwenye mji wa Cianjur ambao ndio uliokuwa chanzo cha tetemeko lililosababisha maporomo ya ardhi, mapaa na kuta kuanguka na kuzikwa kwa wahanga.

Athari za tetemeko la ardhi. Picha ya GETTY IMAGES.

Makumi ya wahanga, walitumia siku nzima ya jana (Alhamis ya Novemba 24, 2022), kujaribu kumuokoa binti huyo wakitumia vifaa vya kuchimbia na hata mikono yao katika zoezi lililositishwa usiku na mapema hii leo, msichana huyo amepatikana akiwa amefariki.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 26, 2022
Tunajenga Chuo cha Mafuta, Gesi na Umeme: Makamba