Mahakama ya kitamaduni nchini Zimbabwe imemtaka mke wa Hayati Robert Mugabe, Grace Mugabe kufika mbele ya mahakama hiyo kufuatia shtaka la kukiuka kanuni za mazishi ya Mwili wa mumewe.

Mjane huyo anadaiwa kukiuka tamaduni kwa kumzika mumewe nyumbani (homestead) badala ya eneo lililochaguliwa na ndugu na Mama wa marehemu.

Hata hivyo barua kutoka kwa Chief Zvimba, Chief wa eneo alikozaliwa Rais Mugabe, kwenda kwa Grace imemuelekeza mjane huyo kufukua mwili huo ili uzikwe upya kwa mujibu wa taratibu za watu wa Zvimba.

Sambamba na hayo Mjane Grace ametakiwa kulipa faini ya ng’ombe na mbuzi kwa kukiuka tamaduni.

Mugabe alifariki dunia mwaka 2019 nchini Singapore akiwa na umri wa miaka 95 na alizikwa katika eneo la Katuma, Wilayani Zvimba baada ya mvutano kati ya Serikali na familia kuhusu eneo la kumzika.

Mmoja wa wanafamilia amenukuliwa akisema kuwa mazishi ya Mugabe yalizingatia matakwa yake, na kuwa hakuna mgogoro ndani ya familia hivyo jambo hilo lipo juu ya mamlaka ya Chief.

Madereva watwangana ngumi
ACP Marwa: Wawafikishe waharifu kwetu