Mwili wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad umewasilili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, mjini Unguja na kuagwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja mjini Unguja.

Baada ya kuswaliwa, mwili wa Maalim Seif umesafirishwa kwenda kisiwani Pemba kwa ajili ya mazishi leo jioni katika eneo la Mtambwe ambako atazikwa.

Mapema leo Asubuhi mwili wa Maalim Seif uliswaliwa katika Msikiti wa Masjid Maamur Upanga jijini Dar es Salaam, kisha kusafirishwa hadi Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya safari ya kuelekea Zanzibar.

Maalim alifariki dunia jana Februari 17 katika hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Polisi TZ yalikataa kwata la JKT TZ
Seif Kombo akubali yaishe