Dar es Salaam. Mwili wa aliyekuwa katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata),  Godfrey Mngereza utawasili  Dar es Salaam Jumatatu Desemba 28, 2020.

Taarifa iliyotolewa na Basata inaeleza kuwa mwili utaagwa Jumanne ukumbi wa Karimjee na mazishi yatafanyika Desemba 30, 2020 kijijini kwao Suji wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Inaeleza kuwa kwa sasa msiba upo nyumbani kwa marehemu Kibamba Luguruni jijini Dar es Salaam.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa Dodoma , Ernest Ibenzi amesema tangu afikishwe hospitali Desemba 22 hali yake haikuwa nzuri jambo liliwalazimu kumuweka chumba cha uangalizi (ICU) na alifariki dunia akiwa katika chumba hicho.

Wawili wapoteza maisha kuporomoka kwa jengo la Beit Al Ajaib
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 26, 2020