Mwili wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe aliyefariki dunia  Septemba 6, 2019 leo unasafirishwa kurejeshwa nyumbani kutoka Singapore ambapo alikuwa akipatiwa matibabu tangu Aprili mwaka huu kutokana na maradhi ambayo yalikuwa yakimsumbua ikiwa pamoja na umri.

Mugabe ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 ameiongoza nchi hiyo kwa miaka 37 mara tu baada ya nchi hiyo kupata uhuru 1980 hadi alipong’olewa madarakani 2017.

Emmerson Mnangagwa aliteuliwa kuongoza Zimbabwe baada ya Mugabe kuondolewa madarakani.

Mugabe katika harakati zake  za uhuru amewahi kuwekwa  jela kwa muda wa miaka 10 bila ya kufunguliwa mashtaka kwa kukosoa uongozi  katika kipindi cha miaka ya 1964.

Mnamo mwaka  1973, Mugabe alichaguliwa kuwa  katibu wa chama cha ZANU PF.

Robert Mugabe atakumbukwa kwa mengi  katika ukanda wa Afrika Kusini na bara la Afrika.

Aidha serikali imethibitishwa kuwa mazishi yake yatafanyika katika siku mbili za wikendi ijayo ambapo kitaifa mwili wake utaagwa siku ya Jumamosi kabla ya kuzikwa kijijini kwao jumapili.

 

 

 

 

 

Wawekezaji kutoka Rwanda watua Kagera kuchangamkia fursa ya kilimo na ufugaji
Neymar kupigwa bei Januari 2020