Hatimaye Mwili wa marehemu Mzee Francis Maige Kanyasu umeagwa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kusafirishwa na Serikali kwenda kijijini kwao Igokero wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
 
Akizungumza katika Shughuli hiyo ya kuuaga mwili huo, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamaii , Jinsia , Wazee na Watoto, Marcel Katemba amesema kuwa mzee Kanyasu atakumbukwa milele kwa mchango wake alioutoa enzi za uhai wake.
 
“Nawapongeza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa juhudi zenu ni kweli mlitaka kuokoa maisha ya mzee wetu, lakini kazi ya Mungu haina makosa , pia sina budi kuwashukuru majirani zake na uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Malapa kwa kujitoa naomba mfanye hivyo hata kwa wazee wengine’’ amesema Katemba.
 
Hata hivyo, kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya dharura na Ajali, Dkt. Juma Mfinanga amesema walimpokea Mzee Kanyasu Mei 25, 2017 akitokea Hospitali ya Amana alikokuwa akipatiwa matibabu na walipomfanyia vipimo vya awali waligundua anasumbuliwa na maradhI ya Kifua Kikuu ambayo alikuwa nayo kwa muda mrefu kutokana na mazingira aliyokua akiishi.

ANC wataka Rais Zuma achunguzwe tena, washindwa kumtetea
Marekani yaigeuzia ubao China, yatoa onyo kali