Amani ni neno lenye herufi chache lakini lina uzito mkubwa katika uhusiano wa jamii, hivyo viongozi wana wajibu wa kulinda nguzo hiyo kwa kizazi cha sasa na kijacho, lakini pia viongozi wa dini wanajukumu la kuhubiri amani katika majukwaa mbalimbali kwa kuwa ni nguzo endelevu kwa kizazi kijacho.

Hayo yamezungumzwa na Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi wakati wa mkutano wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es salaam, uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Katika mkutano huo baadhi ya viongozi wa dini wamesema kuwa haijalishi tofauti zilizopo katika jamii la msingi ni kuvumiliana na kuungana katika ulinzi wa amani.

”Moto mkubwa huanza kwa cheche, Serikali haitakiwi kupuuza cheche zinazoonekana kwa sasa na badala yake iziondoe” Maneno hayo yamezungumzwa na viongozi wa dini katika mkutano huo.

Aidha Askofu wa Kanisa sla Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam, Jackson Sosthenes ametaja baadhi ya athari za kuharibu amani kuwa ni pamoja na kuathirika kwa wanyonge na kukosa uhuru wa kuwa na mikusanyiko.

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amewaomba viongozi wa dini kutumia majukwaa kuhubiri amani.

 

Tanapa yasitisha shughuli za utalii
John Cena abwagana na mchumba wake