Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua Mwenyekiti wa Chama cha ACT – Wazalendo na aliyekuwa Mgombea urais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Awali chama hicho Kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar kilikataa kuyatambua matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa kusema kwamba yalikua batili.

Hata hivyo chama hicho kimeongeza kwamba baada ya majadiliano ya muda mrefu pamoja na kupokea maoni ya wanachama wake, kimeamua kuungana na serikali ya chama tawala kwa ajili ya kuendesha nchi.

Jana Desemba 6, 2020 Kamati kuu ya Chama cha ACT – Wzalendo ilitangaza kuridhia kushiriki kwenye serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na kuielekeza Kamati ya Uongozi kupendekeza jina la Mwanachama atakayekuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Aidha kamati hiyo ilitangaza kuwaruhusu wajumbe wa Baraza la wawakilishi, Wabunge na Madiwani waliochaguliwa katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, kwenda kukiwakilisha chama hicho na wananchi waliowachagua.

Jesé Rodríguez avunjiwa mkataba PSG
Wanaume kutawala Bunge la Kuwait