Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amesema katika kipindi kifupi alichokaa madarakani amebaini ubadhirifu wa fedha za umma katika taasisi za serikali.

Mwinyi amebainisha hayo leo Desemba 29, 2020 katika maadhimisho ya siku ya maadili na haki za kibinadamu yaliyofanyika visiwani humo ambapo ameeleza kuwa fedha nyingi za miradi ya maendeleo hazijatumika vizuri.

Kutokana na makosa hayo, Mwinyi amesema serikali yake haitosita kuwachukulia hatua wale wae watakaobainika kuhusika na ubadhirifu huo.

“Lakini kipindi kifupi sana nilichokuwa naangalia taasisi mbalimbali, makosa ni mengi, ubadhirifu ni mwingi, wizi ni mwingi tukisema tukisema tusichukue hatua kwa sababu tunaoneana aibu hatutokwenda popote,” amesema Mwinyi.

Aidha Rais Mwinyi ameagiza ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za Zanzibar kuongeza juhudi katika kusimamia matumizi ya fedha za umma katika taasisi za serikali ili kuziba mianya ya upotevu wa fedha.

Wabunge wa Republican wafungua kesi dhidi ya Pence
Azam FC kusajili wengine wawili