Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameibuka na kuzingumzia rasmi tetesi zinazosambaa zinazomuhusisha kujiunga na klabu ya Azam.

Zahera amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote na hajafanya mazungumzo yoyote mpaka sasa na viongozi wa Azam FC.

Aidha, tetesi za kocha Zahera kuwaniwa na Azam FC zilianza kusambaa mara tu baada ya klabu hiyo kumfukuza kocha wake, Hans van der Pluijm pamoja na kocha msaidizi, Juma Mwambusi kufuatia matokeo mabaya ya mechi za hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Azam FC, Kutokana na mabadiliko hayo ya haraka, kwa sasa benchi la ufundi la Azam FC litasimamiwa kwa muda na makocha wa timu za vijana za timu hiyo, Meja Mstaafu Abdul Mingange (Azam U-20) na Idd Nassor Cheche (Azam U-17) hadi hapo kocha mkuu atakapotangazwa rasmi.

Hata hivyo, Mwinyi Zahera ni moja ya makocha ambao Azam FC inafanya naye mazungumzo kwaajili ya kuchukua mikoba ya kocha Hans van der Pluijm.

Ahadi zote alizoahidi JPM zitatekelezwa- Majaliwa
Korosho bado kaa la moto, wakulima wanena, 'Hatuelewi hatma yetu'