Mwaka 2022 unaingia kwenye rekodi ya kuzika ugomvi baina ya msanii mahiri wa hip hop kutoka nchini Marekani 50 cent pamoja na mwanamasumbwi mahiri duniani Floyd Mayweather.

Wawili hao ambao hawakuwa katika maelewano mazuri kwa kipindi kirefu huku kila mmoja kwa wakati wake akijigamba na kuwadhihirishia mashabiki zao kuwa bora zaidi ya mwenzake.

Rapa 50 cent amedhihirisha ukomo wa bifu hilo jana Agosti 14, 2022, baada ya kuchapisha picha ya Floyd Mayweather kupitia ukurasa wake wa Instagram aliyoiambatanisha na ujumbe unaothibitisha kuwa Floyd Mayweather atakuwa mmoja wa watu mashuhuri watakaohudhuria kwenye sherehe yake aliyoipa jina la ‘Tycoon’ itakayofanyika mapema Agosti mwaka 2022.

Floyd Mayweather na 50 cent mara kadhaa habari zao zimekuwa zikishika nafasi kwenye vyombo mbali mbali vya habari duniani kufuatia wawili hao kurushiana maneno makali na vitisho kupitia kwenye mitandao yao ya kijamii na katika mahojiano tofauti.

Kuna wakati rapa 50 cent aliomba liandaliwe pambano maalum ili wawili hao waingie ulingoni kufundishana adabu.

50 Cent na Floyd Mayweather hapo awali walianza kama marafiki wazuri na washirika wa kibiashara hadi mwaka 2012, ambapo vyanzo vimewahi kueleza kuwa ugomvi wao ulianza muda mfupi baada ya Mayweather kuachiliwa huru kutoka gerezani ambapo 50 alidai kwamba alikuwa akimdai pesa, deni lililoanza muda mfupi baada ya rapa huyo kuanza kufanya kazi na The Money Team.

Mafuriko yauwa 31, wengi ni Wanawake na Watoto
Kenya: Ngome pinzani zaanza sherehe kabla ya matokeo