Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita leo Februari 11, 2018 ameungana na wakazi wa jijini Dar es salaam katika kongamano la kupima Magonjwa ya Kisukari na Presha lililoandaliwa na Lions Clubs International kwa kushirikiana na Kituo cha Afya cha Irania  kilichopo jijini hapa.

Katika kongamano hilo Meya Mwita amewapongeza waandaaji na kuwaeleza kuwa wasiishie hapo hivyo wafikishe huduma hiyo kwenye halmashauri nyingine za jiji la Dar es Salaam ili wananchi wote waweze kupata huduma hiyo.

“Jambo hili ni muhimu sana, ninawapongeza, ombilangu kwenu angalieni namna ya kuendelea kuwasaidia wananchi wengine katika jiji letu la Dar es Salaam, huduma hii ni ya muhimu sana na kila  mwananchi anahitaji kuipata” amesema Meya Mwita.

Meya Mwita amesisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kucheki afya zao hususani inapojitokeza fursa hizo kwa kuwa baada ya kupata majibu ya vipimo hivyo inawapa urahisi katika kupata matibabu.

Amesema Taasisi hizo zimekuwa na mchango mathubuti  kwa wananchi kutokana na uzalendo mkubwa waliokuwa nao na hivyo kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo.

Awali akimkaribisha Meya Mwita, Rais wa Lions Clubs Shaheen Alam amempongeza na kumueleza kuwa  wamekuwa wakitoa huduma hiyo kwa kushirikiana na Kituo cha Afya cha  Iranian kwa lengo la kuwasaidia wananchi kutambua afya zao.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 12, 2018
Ndege yenye abiria 71 yaanguka baada ya kupoteza mawasiliano

Comments

comments