Meya wa Jiji la Dar es salaam Isaya Mwita, amesema kuwa wanaendelea kukamilisha ukarabati wa awali wa miundo mbinu ya Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo (UBT).

Mwita, amesema kuwa ukarabati huo ulikuwa ukihusisha uboreshaji miundo mbinu ya kuegesha magari, vyoo,uwekaji sakafu ndani ya kituo na ufungaji taa ndani ya kituo hicho.

“Tunaendelea kukamilisha ukarabati  wa kituo cha Ubungo hasa maeneo ya maegesho ambayo yamefanyiwa maboresho, vyoo na ndani ya kituo taa zimefungwa”amesema Mwita.

Aidha, Mwita amesema kuwa baada ya kumalizika kwa ukarabati huo wa awamu ya kwanza, wataendelea na uwekaji uzio imara wa kituo hicho, huku akisisitiza kuwa lengo lao ni kuwasaidia abiria wa ndani na nje kupata huduma wakiwa kituoni hapo.

Hata hivyo ameongeza kuwa mchakato wa ukarabati utakapo kamilika utafungua fursa za uwekezaji  wa kibiashara kwa wafanyabiashara wa ndani na nje

Suala La Mchezaji Hassan Ramadhani Kessy
Serikali yatenga sh. bil.15 kutoa mafunzo kwa vijana zaidi 2,500