Kiungo mpya wa Simba, Mzamilu Yasin aliyetokea Mtibwa Sugar ametamba kuwa suala la kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo halina tatizo na wala hatishwi na uwepo wa Jonas Mkude katika nafasi hiyo.

Mzamilu aliyesajiliwa hivi karibuni kwamkataba wa miaka miwili pia alieleza atajitolea zaidi kuisaidia Simba msimu ujao ili irejee kwenye njia yake na kukata kiu ya makombe klabuni hapo.

“Nacheza nafasi zote za viungo ila napenda zaidi namba nane, namheshimu Mkude na viungo wengine Simba lakini nikiri kuwa sina hofu ya namba kwenye kikosi cha kwanza kwa sababu hakuna kikosi utakachokwenda ukakosa changamoto ila kwa kuwa naiamini kazi yangu, hilo litakuwa jepesi, sina wasiwasi.

Mzamilu pia amesema hatishwi na uwepo wa viungo wengi klabuni hapo akiwemo Justice Majabvi, Said Ndemla, Awadh Juma, Mwinyi Kazimoto, Peter Mwalyanzi na Mkude kwa kuwa yeye ni mpambanaji na anaiamini kazi yake.

“Lakini niseme pia nina imani kubwa Simba itafanya vizuri msimu ujao kutokana na usajili wanaoendelea kuufanya, ukichanganya na wachezaji tutakaowakuta itakuwa ni timu nzuri na nina imani viongozi pia watajipanga vya kutosha kwa ajili ya kuipa mafanikio timu msimu ujao,” alisema Mzamilu.

Ronald Koeman Kumrudisha Luis Nani England
Jose Mourinho Aichokonoa Arsenal