Mlinda mlango Daniel Mgore ameweka rekodi ya kipekee kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2020/21, baada ya kuwa mlinda mlango pekee aliekubali kufungwa mabao mengi katika mchezo mmoja, huku akikataa kuruhusu nyavu zake kutikiswa kwenye michezo mingine.

Mlinda mlango huyo wa klabu ya Biashara United Mara alikubali kufungwa mabao manne, wakati wa mchezo dhidi ya Mabingwa Watetezi Simba SC uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam mwanzoni mwa mwezi huu.

Mgore mpaka sasa ameshacheza michezo sita, na hajaruhusu bao katika michezo mitano (ana Cleen Sheet tano).

Licha ya kwamba Biashara United imeshinda michezo minne na kulazimisha sare moja ya bila kufungana na Ruvu Shooting,  Septemba 27, bado mwendo wa safu yao ya ushambuliaji ni bao moja kwa kila mchezo walioshinda.

Mwenendo wa klabu hii ya mjini Musoma mkoani Mara:

Biashara United 1-0 Gwambina, Septemba 6, Uwanja wa Karume.

Biashara United 1-0 Mwadui, Septemba 13 Uwanja wa Karume.

Simba 4-0 Biashara United, Septemba 20 Uwanja wa Mkapa.

Ruvu Shooting 0-0 Biashara United,  Septemba 27 Uwanja wa Mabatini.

Biashara United 1-0 Mtibwa Sugar, Oktoba 4 Uwanja wa CC Kirumba.

Biashara United 1-0 Ihefu. Oktoba 14 Uwanja wa Karume.

Kwa matokeo hayo Biashara United Mara ipo nafasi ya nne kwa kufikisha alama 13, kinara ni Azam FC akiwa na alama 18 baada ya kucheza mechi sita msimu wa 2020/21.

Katwila: Nawashukuru Mtibwa Sugar
Simba SC yaifuata Prisons, Mugalu akabidhiwa fupa