Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Amri Athuman maarufu kwa jina la Mzee Majuto amewatoa wasiwasi wapenzi na mashabiki wake kuwa yeye ni mzima kabisa na endapo Mungu atamchukua ‘kufariki’ basi watapata habari popote pale watakapo kuwepo.

Majuto ametoa kauli hiyo baada ya siku za hivi karibuni kuzushiwa kifo kwa mara nyingine tena baada ya yeye kuzidiwa na kurudishwa hospitalini kwa mara nyingine ili aweze kupatiwa matibabu juu ya ugonjwa unaomsumbua.

Mimi ni mzima kabisa, watu msiwe na wasiwasi kama nikifa mtapata habari nyote kwamba mimi tayari nimeshaaga dunia na sina wasiwasi kwa sababu wazazi wangu wote hawapo, mtume wangu ninayempenda Mohamed (S.A.W) naye pia hayupo sasa sembuse mimi msihofu sana jamani,”amesema  Mzee Majuto

Hata hivyo,  siku ya Jumatatu Aprili 23, 2018 Mzee Majuto alilazwa katika Hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam, baada ya kuzidiwa. Awali Majuto alilazwa hospitalini hapo mnamo Januari mwaka 2018 na kufanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa tezi dume ambao ndio umekuwa ugonjwa wake mkubwa unaomsumbua kila mara.

 

 

Tanzia: Lady Jaydee apata pigo
Kim Jong-un kuweka rekodi mpya na Korea Kusini kesho

Comments

comments