Mwigizaji wa kikundi cha maigizo cha Kashkashi kinachorusha mchezo wao wa kuchekesha wa Mizengwe kupitia kituo cha ITV, Jumanne Alela maarufu kama Mzee Matata amefariki dunia  usiku wa kuamkia leo Juni 16, 2021.

Mzee Matata amefariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, alipokuwa amelazwa kwa matibabu tangu Juni 13, 2021..

Kwa mujibu wa mwigizaji maarufu nchini, Madebe Lidai, mazishi ya Mzee Matata yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Buguruni –Malapa jijini Dar es Salaam.

“Mazishi ya Mwanatasnia mwenzetu Mzee Jumanne Alela (Mzee Matata) yatafanyika kesho saa saba mchana kwenye Makaburi ya Buguruni-Malapa.

“Msiba upo kwa ndugu zake, Chamazi kwa Mkongo (jijini Dar),” imesema taarifa kutoka kwa Madebe Lidai.

Nabi kutema tisa, kusajili wanane
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 16, 2021