Mbunge wa Jimbo la Mtama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa IPP Media, Dkt. Reginald Mengi hakuwa mbaguzi kwa wanasiasa wa vyama vyote.

Ameyasema hayo mkoani Kilimanjaro wakati wa Ibada ya kuaga mwili wa marehemu Dkt. Reginald Mengi ambapo amesema kuwa mchango wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM ulikuwa ni mkubwa.

Amesema kuwa Dkt. Mengi alikuwa habagui wanasiasa kwani hata wale wa upinzani aliwasaidia, hata Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2015 alishiriki kwenye kuiandika huku akisaidia kutoa mawazo kwenye sera ya kiuchumi ya Umoja wa vyama vya upinzani UKAWA

”Mengi alikuwa wa kipekee na pengine asingekuwa Mfanyabiashara angeweza kuwa kiongozi wa Dini kwani upendo wake haukuwa wa kawaida, amewasaidia watu wengi wenye ulemavu na watu wenye uhitaji,”amesema Nnauye

Mengi aliniunga mkono kwenye mbio za Urais- Benard Membe
Viongozi wa upinzani nchini Uganda watangaza kumng'oa Museveni

Comments

comments