Ni hali isiyokuwa ya kawaida kwa binadamu kufika umri mrefu akiwa hai, lakini leo linathibitika kwa mara nyingine nchini Tanzania katika Kitongoji cha Ing’enyango nje kidogo ya kijiji cha Kilosa wilayani Mufindi mkoani Iringa kilomita 70 kutoka mji wa Mafinga ambapo Dar24 imempata mzee  Silyamgoda Kalinga mwenye umri wa miaka 140.

Mzee Silyamgoda amesema ameitaka jamii kuwaenzi wazee wenye umri mkubwa na kuhitaji msaada kutokana na umri wake.

Akizungumza na Dar24 mtoto wa mzee huyo, Paskari Kalinga amesema kuwa mzee wake alizaliwa mwaka 1879 na ana watoto wanne, wajukuu zaidi ya mia moja, vitukuu 65 na vilembwe 35 huku akikabiliwa na changamoto kubwa kwani haweze kuona, kutembea pamoja na kuongea vizuri jambo linalochangiwa pia na maradhi mbali mbali yanayomsumbua kutokana na uzee wake.

“Huyu ni baba wa mimi siwezi kwenda hata sehemu tupo na mama ambaye nimeolea Iringa, wenzetu wanaogoma kulea tunawaacha tu avayago ve valema valekage (aliongea kwa lugha ya kihehe) lakini mpaka leo mimi na mke wangu bado tupo mpaka leo tunamhudumia, huyu mzee kitu kinachokwama ni chakula hamna, nguo pia hamna yaani kila kitu nafanya peke yangu na uwezo wangu ni mdogo” alisema Paskari.

Naye Mke wa Paskari (Mkwe wa mzee Silyamgoda) amesema kuwa alianza kumlea mzee huyo tangu mwaka 1995 mpaka sasa licha ya kuwa na maisha magumu.

“Huyu mgonjwa mimi nilimkuta toka 95 mwezi watatu akiwa na mama mkwe nilikaa nao kidogo tu baada ya miaka mitatu mama mkwe akafa nimeendelea kumtunza huyu mpaka sasa ila nimeachiwa huwa nalala humu ndani peke yangu hakuna mtu anayekuja kufua nguo wala kumuogesha ni mimi peke yangu” alisema mke wa Paskari Kalinga.

Licha ya kujifunza maisha ya mzee huyo ambaye siri kubwa ya kuishi miaka mingi ni kutokana na chakula cha asili anachokitumia kwa miaka yake yote lakini ameiomba Serikali ya Tanzania iweze kumsaidia kwani mazingira anayoishi siyo rafiki kiafya.

Video: Rais Magufuli ateua viongozi hawa leo
Video: Spika Ndugai amtisha CAG, Lugola ashtukia wahalifu

Comments

comments