Mzee mmoja aliyefahamika kwa jina la Laurian Kakoto (80) mkazi wa Kijiji cha Ihunga Kata ya Kishanda mkoani Kagera amekutwa ameuawa kikatili na kuzikwa kwa kutanguliza kichwa akiwa amekatwa koromeo na kuondolewa sehemu za siri.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 08/01/2019 kwa kuhusishwa na imani za kishirikina ambapo mwili wa marehemu Kakoto ulikutwa umefukiwa kwenye shimo la mita moja kwenye shamba la mahindi.

Hata hivyo, Kamanda Malimi amesema kuwa marehemu aliondoka nyumbani kwake tarehe 7,Januari,2019 kwenda kununua mchele na unga ambapo kando ya shimo ulipofukiwa mwili wa marehemu kulikutwa mfuko wa mchele, huku akisema msako dhidi ya watuhumiwa unaendelea.

FBI yaitahadharisha Ikulu ya Marekani 'White House'
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 12, 2019

Comments

comments