Mbubiri maarufu wa kanisa la Maombezi la GRC lililoko Ubungo jijini Dar es Salaam, Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako, amesema waandishi wote wa habari waliomuandika vibaya watakufa kabla ya Machi Mwakani.

Akizungumza wakati wa mahubiri yake jana Jumapili kanisani humo, ikiwa zimepita wiki nne baada ya kupata tuhuma za kunywa pombe na kumtukana jirani yake, Mzee wa Upako ameahidi kuachana na kazi ya kuhubiri endapo waandishi hao hawatakufa katika kipindi alichotabiri.

“Kila mwandishi aliyeniandika vibaya ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe,” Mzee wa Upako anakaririwa na Mwananchi.

Alisema kuwa anaamini waandishi walioandika habari hizo alizodai za kumchafua walikuwa wamehudhuria ibada hiyo, hivyo ujumbe wake umefika.

Wiki iliyopita, Mzee wa Upako alikanusha taarifa za kuwa alikuwa amekunywa pombe akitaka ielezwe alikunywa pombe gani na kiasi gani.

 

Video: Panga latua wanufaika 'dili' watumishi hewa, Wingu zito kupotea msaidizi wa Mbowe...
Wasira: Sijateuliwa kuwa msemaji wa CCM